Ezekiel 24:3-13

3 aIambie nyumba hii ya kuasi fumbo, na uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Teleka sufuria jikoni; iteleke
na umimine maji ndani yake,
4 bWeka vipande vya nyama ndani yake,
vipande vyote vizuri,
vya paja na vya bega.
Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri;
5 cchagua yule aliye bora wa kundi la kondoo.
Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa;
chochea mpaka ichemke
na uitokose hiyo mifupa ndani yake.
6 d“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ole wa mji umwagao damu,
ole wa sufuria ambayo sasa
ina ukoko ndani yake,
ambayo ukoko wake hautoki.
Kipakue kipande baada ya kipande,
bila kuvipigia kura.

7 e“ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake:
huyo mwanamke aliimwaga
juu ya mwamba ulio wazi;
hakuimwaga kwenye ardhi,
ambako vumbi lingeifunika.
8 fKuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi,
nimemwaga damu yake
juu ya mwamba ulio wazi,
ili isifunikwe.
9 g“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ole wa mji umwagao damu!
Mimi nami nitalundikia kuni nyingi.
10Kwa hiyo lundika kuni
na uwashe moto.
Pika hiyo nyama vizuri,
changanya viungo ndani yake,
na uiache mifupa iungue kwenye moto.
11 hKisha teleka sufuria tupu kwenye makaa
mpaka iwe na moto sana na shaba yake ingʼae,
ili uchafu wake upate kuyeyuka
na ukoko wake upate kuungua na kuondoka.
12Imezuia juhudi zote,
ukoko wake mwingi haujaondoka,
hata ikiwa ni kwa moto.
13 i“ ‘Sasa uchafu wako ni uasherati wako. Kwa sababu nilijaribu kukutakasa lakini haikuwezekana kutakaswa kutoka kwenye huo uchafu wako, hutatakasika tena mpaka ghadhabu yangu dhidi yako iwe imepungua.

Copyright information for SwhNEN